KULALA KUPOOZA
By Bernadetha Bwire
Ilikuwa Ijumaa usiku hali ya ajabu,ya kutisha na ngumu kuelezea iliponitokea wakati tu ninaanza kupata usingizi. Mara tu nilipoanza kupata usingizi nilimuona msichana nisiyeweza mtambua sura,akinisogelea nilipokuwa nimelala, akanikaba shingoni nilijawa na woga sana na nilipojaribu kuamka nilishindwa kwasababu ya uzito uliokua juu ya mwili wangu. Baada ya kuamka na kusimulia wanafunzi wezangu baadhi waliniambia ni jinamizi la usiku wakihusianisha hali ile na jini, wengine wakisema ni watu wa nguvu za giza wanakuchezea na wakinishauri njia mbalimbali za kufanya kuepukana na nguvu hizo ikiwemo kuombewa kanisani. Tangu siku hiyo hali ile ilizid jirudia mara kadhaa na akili yangu haikuridhika na majibu niliyopewa kuhusu hali hii, baada ya kusoma makala na vitabu ndipo nilipokutana na neno kulala kupooza yani Sleeping paralysis.
Ilikuwa Ijumaa usiku hali ya ajabu,ya kutisha na ngumu kuelezea iliponitokea wakati tu ninaanza kupata usingizi. Mara tu nilipoanza kupata usingizi nilimuona msichana nisiyeweza mtambua sura,akinisogelea nilipokuwa nimelala, akanikaba shingoni nilijawa na woga sana na nilipojaribu kuamka nilishindwa kwasababu ya uzito uliokua juu ya mwili wangu. Baada ya kuamka na kusimulia wanafunzi wezangu baadhi waliniambia ni jinamizi la usiku wakihusianisha hali ile na jini, wengine wakisema ni watu wa nguvu za giza wanakuchezea na wakinishauri njia mbalimbali za kufanya kuepukana na nguvu hizo ikiwemo kuombewa kanisani. Tangu siku hiyo hali ile ilizid jirudia mara kadhaa na akili yangu haikuridhika na majibu niliyopewa kuhusu hali hii, baada ya kusoma makala na vitabu ndipo nilipokutana na neno kulala kupooza yani Sleeping paralysis.
HISTORIA FUPI SANA KUHUSU HALI HII KATIKA JAMII MBALIMBALI.
Katika nchi ya Tanzania watu wengi huita hali hii majinamizi ya usiku wakiamini kuwa husababishwa na jini anayemtembelea mtu pindi amelala usingizi akiwa na lengo baya, wengine huhusianisha hali hii na majini mahaba wakiamini hutembelea watu ili KUIFANYA nao tendo la ndoa. Ili kujikinga na hali hii baadhi ya watu hufunga mkaa kwenye shuka la kujifunika, huku wengine wakichungulia uvungu wa kitanda kabla ya kulala ili kumfukuza pepo huyo na wengine hukemea kwa maombi.
Sio tu Tanzania tu wenye imani hii kwani nchini Mexico hali hii huitwa "Se Me Sio El Muerto" ikimaamisha mwili wa mtu aliyekufa juu yangu huku wakihusianisha na roho waovu yaani mashetani. Katika nchi ya Japani hali hii huaminika kusababishwa na roho waovu wanaotaka kulipiza kisasi kwa watu waliofanya makosa huku wakiita "Kanashibiri". Katika baadhi ya nchi za Magharibi hali hii iliaminika sana kusababishwa na majini wanaotembelea watu ili kufanya nao tendo la ngono na wakifika husababisha uzito unaowafanya wahusika wasishindwe sogeza miili yao huku jini wa kiume alijulikana kama Incubus na wakike Succubus.
MAELEZO YA KISAYANSI KUHUSU KULALA KUPOOZA.
Kwa mujibu wa Ryan Hurd kwenye makala yake ya "The sleeping paralysis report" kulala kupooza ni hali impatayo mtu pale muingiliano wa taswira za kwenye mazingira ya ndoto kutokea katika mazingira ya mtu akiwa macho au anaufahamu na mazingira yake halisi au ya nje ya usingizi(ndoto).Kwa kifupi ni hali impatayo mtu pale ubongo au akili yake ikiwa macho lakini mwili wake umelala au kupooza. Kulala kupooza au sleeping paralysis humpata mtu pindi tu anaanza kupata usingizi (wakati akiwa ubongo wake ukiwa bado na ufahamu na mazingira yake yamzungukayo) au humpata mtu pindi tu anapotaka kuamka kutoka usingizini ( akiwa tayari ubongo wake umeanza rejea ufahamu wa mazingira yake ya nje au halisi) na hivyo kumfanya mtu huyo ashindwe kujisogeza mwili wake na kupatwa maono (hallucinations) ya taswira mbalimbali.
JE NI NINI HASA KITOKEACHO WAKATI WA KULALA KUPOOZA?
Kwa mujibu wa kitabu cha "Principle of physiology" cha Leesey, kulala kupooza ni sifa mojawapo ya Rapid eye Movement sleep (REM) ambayo ni moja ya hatua za usingizi. Kwa mujibu kwa hichohicho kitabu kuna hatua nne za usingizi ambapo hatua ya kwanza hadi ya nne zipo ndani ya Non rapid eye movement (NREM) baada ya hatua hizo hufuatia mfululizo(episode) wa REM sleep ambao hujirudia mara tano katika mzunguko mzima wa usingizi. Ndoto tuziotazo hutokea katika sura ya tatu na ya nne ya NREM sleep na pia hutokea katika REM.
Patrick McNamara, Patricia Johnson, Erick Harris, Catherine Baeuharnais na Sanford Auerbach katika makala yao ya "REM na NREM sleep mentation" wamenukuu kwamba ndoto zitokeazo katika hatua ya NREM sleep ni tofauti na ndoto zitokeazo katika hatua ya REM sleep kwani katika utafiti uliofanywa inaonesha kuwa ndoto ziotwazo katika hatua ya NREM sleep ni ndoto zinazohusiana na mazingira rafiki ya muingiliano wa kijamii wa mhanga na jamii yake na ndoto hizo hutokea katika mazingira halisi, ya kawaida tuishio kila siku. Lakini hatua hii ya REM sleep ndoto ziotwazo katika hatua hii ni zile zinazohusisha mazingira ya ugomvi na yasiyo rafiki ya muingiliano wa kijamii na ndoto zinazofanyikia hapa zinaleta taswira za kutisha na mazingira yake yanaweza kuwa yale ya kawaida au mazingira yasiyo ya kawaida. Na kwa mujibu wa hiyohiyo makala ndoto zitokeazo katika hatua hii ya REM sleep ndio ndoto nyingi zitokeazo hapa husababishwa na mwingiliano au mawasiliano ya kijamii (yale mambo tunayokutana nayo katika jamii)kuliko ndoto tuotazo katika hatua ya NREM sleep.
Pia kwa mujibu wa kitabu cha Principle of physiology , katika hatua ya tatu ya NREM mwili wa binadamu huanza kupooza huku shinikizo la damu, joto na kupumua vikishuka kwa kiwango cha chini. Na katika hatua ya nne ambayo sasa mtu huelekea katika REM mwili hupooza sana na ni vigumu kumwamsha mtu kutoka usingizini. Baada ya kuingia katika hatua ya REM sleep, mapigo ya moyo huzidi kwa kiwango cha juu sana, mwili hupooza kasoro macho ambayo huwa yanapepesa pepesa kama mtu anayeangalia Tv, shinikizo la damu, joto pamoja na kupumua huongezeka kwa kiwango cha juu sana na pia ubongo katika hatua hii hutumia hewa ya oxygen zaidi ya mtu aliyeko macho. Kwa mujibu wa tafiti mpya chanzo chuo kikuu cha Toronto, Kupooza huku kwa mwili husababishwa na kemikali mbili Gabab pamoja na glycine ambazo huzuia mfumo wa neva mota (Motor neurone) na kufanya misuli kupooza(paralyse) ili mtu asihangaike hangaike wakati wa hatua hii ya REM (kuota ndoto) na kusababisha kujijeruhi au kumjeruhi jirani.
Pale REM sleep inapotokea wakati usiosahihi na kukuta ubongo wa mlengwa unaufahamu na mazingira yake ya nje ya usingizi au uko macho wakati mwili wake umelala au umepooza ndipo kulala kupooza (sleeping paralysis) hutokea.
Mchanganyiko wa taswira za ndotoni (sababu ya REM/Kuota ndoto wakatiusio sahihi)na uhalisia(unaosababishwa na ubongo kuwa na ufahamu) husababisha mhanga kupatwa na maono (hallucinations) ya kuona viumbe wa ajabu, kusikia sauti, kuona mlango unafunguliwa, kuhisi kukabwa kooni, kuhisi kukaliwa na kiumbe kizito sana juu yake n.k. Na kusababisha mhanga akitoa sauti kujaribu kuita mtu aliyekaribu haitoki, akijaribu kunyanyua mwili hawezi.
Hali hii ya kulala kupooza hutokea katika hatua mbili ya kwanza pale tu mtu anapotaka kuanza kupata usingizi (hypnogogia) na pindi tu mtu anataka kuamka kutoka usingizini (hypnopompia)
Ryan Hurd anasema japokuwa binadamu anauwezo wa kuuhisi mwili na pale alipolala lakini asiweze kujisogeza na macho yake pamoja na milango ya fahamu huwa na taswira ya kama mtu yupo ndotoni, anaendelea kwa kusema ni maajabu kwelikweli kwani hali hii ni zao la hali ya ufahamu ya kuota huku mtu yupo macho kabisaa. Lakini pia Hurd anasema kwa wengi sio miujiza kwani huogopesha sana kwasababu tunabuni kwamba tuko macho na uoga huongezeka na kuongeza taswira za ndotoni na kitokeacho ni kuzalisha kitu chenye taswira mbaya zaidi.
DALILI ZA MTU ALIYEPATWA NA KULALA KUPOOZA.
1)kuhisi kushindwa kujisogeza au kuamsha mwili.
2)kuhisi kukandamizwa kifuani.
3)kuhisi hofu iliyopitiliza.
4)kupumua kwa shida.
5)kuhisi kuona viumbe wa ajabu au mtu anayemtambua/ asiyemtambua.
6)kuhisi kushikwa na kiumbe huyo wa ajabu.
7)Kuhisi kuwa na akili yenye ufahamu (FALSE AWAKE ).
BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA KULALA KUPOOZA.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu ya kulala kupooza ambazo tutazijadili wakati mwingine
1)kutokua na ratiba nzuri ya kulala.
2)Kulalia mgongo.
3)Kuongeza kiasi cha wasiwasi hasa wasiwasi wa mazingira au jamii imzungukayo mhanga.
4) Kuzidisha matumizi ya dawa kama kafeini.
5)Mwili kuchoka sana.
6)Matibabu yatolewayo kwa wagonjwa wa ADHD.
7Kushiba kupitiliza.
8)ugonjwa wa nakolepsi.
9) Athari za galantamine dawa watumiazo wagonjwa wa Alzheimer
Comments