Posts

SONONA/KUSHUKA MOYO

SONONA (DEPRESSION) SI HISIA TU. By Bernadether Bwire " Depression is a prison where you are both a prisoner and a cruel jailer." ~ Anushka Sharma "...  It's like someone turned off the light inside my head...Like always the world around me loses focus and I'm trying to make sense out of it". ~Shaheen Bhatt. Katika maisha kuna nyakati binadamu tunapitia ambapo tunahisi, kuiona na kuifikiria Dunia kama giza nene. Kutokuona muelekeo wa maisha, kutokuhisi hamu ya kufanya chochote na pia kuona hakuna maana ya kuendelea kuishi duniani. Katika nyakati hizi mtu hutawaliwa na mawazo hasi ambayo yakizidi huweza mfanya mtu ajiue. Mawazo hayo hasi huongeza kudhoofika kwa moyo kwani mawazo au fikra hujawa mambo mabaya tu yaliyomtokea mtu, yanayomtokea na pia yatakayomtokea mtu. Mara nyingine si kweli kwamba mtu hukutwa na mambo haya mabaya bali katika nyakati hizi akili ya utambuzi huzibwa na mawazo hasi hivyo kusababisha mtu ashindwe kabisa kuona mwanga katika...

NEUROPLASTICITY

  By Bernadether Bwire. Hii makala imeandikwa kwa ajili ya watu wote kwa dhumuni la kujifunza jinsi ubongo wa binadamu unavyofanya kazi katika nyakati mbalimbali, kuelewa utofauti uliopo kati ya mtu na mtu na hivyo kuufurahia, kuuishi na kuukumbatia.  Jinsi Ubongo unavyobadilika kukabiliana na Mazingira .   Ubongo wa binadamu umejengwa/umeumbwa kwa namna ya kumwezesha aendelee kuishi/kuwepo (survive)  katika nyakati ngumu au kipindi cha hatari. Lara Boyd daktari na pia mtafiti wa mambo yahusianayo na ubongo wa binadamu anasema, "binadamu pamoja na ubongo wake  ulio wa plastiki hujengwa na mazingira yaliyomzunguka".  Na hivyo basi ubongo unasifa ya kubadilika badilika ili kukabiliana na mazingira yamzungukayo mtu. Kila tunapojifunza kitu kipya au ujuzi mpya tunabadili ubongo wetu. Pia kila tunachokifanya, tunachokutana nacho au kukipitia hujenga ubongo wetu na hivyo inaweza kuwa Jambo jema au baya kwetu.  Mabadiliko haya hayana kikomo kwani mabad...

KULALA KUPOOZA

By Bernadetha Bwire Ilikuwa Ijumaa usiku hali ya ajabu,ya kutisha na ngumu kuelezea iliponitokea wakati tu ninaanza kupata usingizi. Mara tu nilipoanza kupata usingizi nilimuona msichana nisiyeweza mtambua sura,akinisogelea nilipokuwa nimelala, akanikaba shingoni nilijawa na woga sana na nilipojaribu kuamka nilishindwa kwasababu ya uzito uliokua juu ya mwili wangu. Baada ya kuamka na kusimulia wanafunzi wezangu baadhi waliniambia ni jinamizi la usiku wakihusianisha hali ile na jini, wengine wakisema ni watu wa nguvu za giza wanakuchezea na wakinishauri njia mbalimbali za kufanya kuepukana na nguvu hizo ikiwemo kuombewa kanisani. Tangu siku hiyo hali ile ilizid jirudia mara kadhaa na akili yangu haikuridhika na majibu niliyopewa kuhusu hali hii, baada ya kusoma makala na vitabu ndipo nilipokutana na neno kulala kupooza yani Sleeping paralysis. HISTORIA FUPI SANA KUHUSU HALI HII KATIKA JAMII MBALIMBALI. Katika nchi ya Tanzania watu wengi huita hali hii majinamizi ya usiku waki...