NEUROPLASTICITY
By Bernadether Bwire. Hii makala imeandikwa kwa ajili ya watu wote kwa dhumuni la kujifunza jinsi ubongo wa binadamu unavyofanya kazi katika nyakati mbalimbali, kuelewa utofauti uliopo kati ya mtu na mtu na hivyo kuufurahia, kuuishi na kuukumbatia. Jinsi Ubongo unavyobadilika kukabiliana na Mazingira . Ubongo wa binadamu umejengwa/umeumbwa kwa namna ya kumwezesha aendelee kuishi/kuwepo (survive) katika nyakati ngumu au kipindi cha hatari. Lara Boyd daktari na pia mtafiti wa mambo yahusianayo na ubongo wa binadamu anasema, "binadamu pamoja na ubongo wake ulio wa plastiki hujengwa na mazingira yaliyomzunguka". Na hivyo basi ubongo unasifa ya kubadilika badilika ili kukabiliana na mazingira yamzungukayo mtu. Kila tunapojifunza kitu kipya au ujuzi mpya tunabadili ubongo wetu. Pia kila tunachokifanya, tunachokutana nacho au kukipitia hujenga ubongo wetu na hivyo inaweza kuwa Jambo jema au baya kwetu. Mabadiliko haya hayana kikomo kwani mabad...