Posts

Showing posts from October, 2019

KULALA KUPOOZA

By Bernadetha Bwire Ilikuwa Ijumaa usiku hali ya ajabu,ya kutisha na ngumu kuelezea iliponitokea wakati tu ninaanza kupata usingizi. Mara tu nilipoanza kupata usingizi nilimuona msichana nisiyeweza mtambua sura,akinisogelea nilipokuwa nimelala, akanikaba shingoni nilijawa na woga sana na nilipojaribu kuamka nilishindwa kwasababu ya uzito uliokua juu ya mwili wangu. Baada ya kuamka na kusimulia wanafunzi wezangu baadhi waliniambia ni jinamizi la usiku wakihusianisha hali ile na jini, wengine wakisema ni watu wa nguvu za giza wanakuchezea na wakinishauri njia mbalimbali za kufanya kuepukana na nguvu hizo ikiwemo kuombewa kanisani. Tangu siku hiyo hali ile ilizid jirudia mara kadhaa na akili yangu haikuridhika na majibu niliyopewa kuhusu hali hii, baada ya kusoma makala na vitabu ndipo nilipokutana na neno kulala kupooza yani Sleeping paralysis. HISTORIA FUPI SANA KUHUSU HALI HII KATIKA JAMII MBALIMBALI. Katika nchi ya Tanzania watu wengi huita hali hii majinamizi ya usiku waki...